Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Juma Kijavara kuhusu hatua iliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa Matanki ya Mafuta yanayojengwa Kigamboni jijini Dar es Salaam, 12 Septemba 2024.
Mkurugenzi wwa Sera na Mipango Maseke Mabiki akisisitiza jambo katika Kikao cha wajumbe wa Menejimenti wa Wizara cha kutoa maoni ya Maboresho ya Sera ya Uchukuzi, kilichofanyika Dodoma.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Naibu Waziri David Kihenzile na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari wakipitia makabrasha wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliowasilishwa na kupitishwa Bungeni 28 Agosti 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania, mara baada ya kufunga Wiki ya Baraza la Usalama lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ludovick Nduhiye akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tanzania (LATRA) hawapo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo hivi karibuni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango (Katikati) katika picha ya pamoja na Mawaziri na Manaibu Waziri mara baada ya kufunguza rasmi mkutano wa siku mbili wa Viongozi, Wataalam na Wadau wa Mazingira kuhusu mwelekeo wa mazingira nchini Septemba 9, 2024.
Katibu Mkuu Prof. Godius Kahyarara akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Maboresho ya Bandari (PIC) hawapo pichani, wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam 11 Septemba 2024.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisisitiza Jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakati kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) jijini Dar es Salaam 1 Agosti 2024.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akihutubia katika hafla ya mapokezi ya Meli ya MV. Annegrit Maiden iliyofanya safari ya Kwanza katika Bandari ya Tanga 30 Julai 2024.