Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Kuhusu Sisi

Wizara ya Uchukuzi  iliundwa tarehe 30 Agosti, 2023 kwa kuzingatia Hati ya Mgawanyo wa Majukumu ya Serikali (Instrument) iliyotolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa hati ya mgawanyo wa majukumu, majukumu ya Wizara ya Uchukuzi ni kama ifuatavyo:

  1. Kuandaa Sera za usafiri na kusimamia utekelezaji wake;
  2. Kuandaa Sera ya Hali ya Hewa na kusimamia utekelezaji wake;
  3. Kusimamia usafiri na usafirishaji kwa njia ya reli;
  4. Kusimamia usafiri na usafirishaji kwa njia ya Anga;
  5. Kusimamia usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji;
  6. Kusimamia utoaji wa leseni za usafirishaji;
  7. Kusimamia utoaji wa taarifa za hali ya hewa kuimarisha usalama hususan katika usafiri kwa njia ya anga na maji; na
  8. Kuongeza tija katika utendaji kazi, kuendeleza rasilimali watu na kusimamia Idara za Serikali, Taasisi, Mashirika ya Umma na miradi iliyo chini ya Wizara ya Uchukuzi.

DIRA

Kuwa nchi yenye huduma za uchukuzi na hali ya hewa zenye uhakika, usalama na nafuu.

DHIMA

Kusimamia na kuwezesha maendeleo ya miundombinu, huduma za uchukuzi na hali ya hewa kwa kutumia sera, sheria na miongozo iliyopo kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.