Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye wakichanganya simenti kuashiria uwekaji wa wa jiwe la msingi wa ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway – SGR) kipande cha Uvinza (Tanzania) hadi Musongati (Burundi), Lot 7&8, Tarehe 16 Agosti,2025 katika eneo la Musongati, nchini Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua usafirishaji wa mizigo kwa kutumia Usafirishaji wa treni ya umeme ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma eneo la Kwala Marshalling Yard mkoani Pwani tarehe 31 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Uchukuzi mara baada ya kuzindua rasmi Bandari Kavu ya Kwala (Kwala Dry Port) iliyopo Kwala, Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani tarehe 31 Julai, 2025.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi mara baada ya kutembelea Bandari ya Tanga 1 Machi 2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakikata utepe kuashiria Mapokezi ya Ndege mpya ya Serikali aina ya B787 Dreamliner mara baada ya ndege hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar mwezi agosti 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za treni ya Reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma 1 Agosti 2024.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora (hawapo pichani) katika uwanja wa Chipukizi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango mkoani humo.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwa na Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mkoa wa Tabora na Chama cha Mapinduzi akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora Oktoba 9, 2024 mkoani Tabora.
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Juma Kijavara kuhusu hatua iliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa Matanki ya Mafuta yanayojengwa Kigamboni jijini Dar es Salaam, 12 Septemba 2024.
Mkurugenzi wwa Sera na Mipango Maseke Mabiki akisisitiza jambo katika Kikao cha wajumbe wa Menejimenti wa Wizara cha kutoa maoni ya Maboresho ya Sera ya Uchukuzi, kilichofanyika Dodoma.