Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

USHIRIKIANO ZAMBIA NA TANZANIA KUIMARISHWA

Imewekwa: 11 Dec, 2025
USHIRIKIANO ZAMBIA NA TANZANIA KUIMARISHWA

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, amezindua reach stacker mpya ya Zambia Cargo and Logistics Limited (ZCL) katika Depo ya Mukuba, Dar es Salaam, na kusisitiza kuimarika kwa ushirikiano wa Tanzania na Zambia katika sekta ya uchukuzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri Kihenzile aliipongeza ZCL kwa kuongeza shehena kutoka TEUs 15,649 mwaka 2021 hadi zaidi ya 40,000 mwaka 2025  ni ishara ya ufanisi na uwekezaji madhubuti katika Miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam.

Naibu Waziri Kihenzile ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha miundombinu ya bandari, reli, barabara na mipaka ili kuboresha biashara kikanda, ikiwamo ujenzi wa SGR, maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam na upanuzi wa Bandari ya Mtwara.

Aidha, ameiomba Zambia kuharakisha ufunguzi wa Nakonde One Stop Border Post ili kupunguza msongamano wa magari Tunduma–Nakonde.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na lojistiki ya Jamhuri ya Zambia Eng. Fredrick Mwalusaka, ambaye alimuwakilisha Waziri wa Wizara ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo yamefanya Kampuni hiyo kuendelea kuongeza mitambo na vifaa mbalimbali ili kuboresha utendaji na tija kwa wateja wanaowahudumia.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya ZCL Joseph Chikolwa amemuhakikishia Naibu Waziri Kihenzile kuwa Kampuni hiyo imeweka mipango madhubuti ya muda mfupi ma mrefu kuhakikisha mzigo unaohudumiwa unaongezeka zaidi ili kuchagiza uchukuzi baina ya Tanzania na Nchi za Ukanda wa Kati.