Muundo
IDARA NA VITENGO
Wizara ya Uchukuzi inaundwa na Idara tano (5) ambazo ni Utawala na Menejimenti ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Sera na Mipango, Miundombinu ya Uchukuzi, Huduma za Uchukuzi na Usalama na Mazingira. Aidha, Wizara hii inaundwa na Vitengo nane (8) ambavyo ni Fedha na Uhasibu, Ufuatiliaji na Tathminini, Mawasiliano Serikalini, Usimamizi wa Ununuzi, Ukaguzi wa Ndani, Huduma za Sheria, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Uchunguzi wa Ajali za Ndege.
TAASISI ZILIZOCHINI YA WIZARA YA UCHUKUZI
Wizara ya Uchukuzi inasimamia jumla ya Taasisi 15, kati ya hizo, Mamlaka za udhibiti ziko nne (4); Taasisi za Utendaji ziko saba (7); Vyuo vya Mafunzo ya kisekta viwili (2); na Mabaraza ya Walaji ni mawili (2). Aidha, kuna vyuo vya Mafunzo ya kisekta vinne (4) vinavyosimamiwa moja kwa moja na Taasisi za kiutendaji. Mchanganuo wa Taasisi hizo ni kama ifuatavyo:
MAMLAKA ZA UDHIBITI
Mamlaka za Udhibiti zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi ni:
- Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA);
- Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA);
- Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC); na
- Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
TAASISI ZA UTENDAJI
Taasisi za kiutendaji zinajumuisha Wakala, Mamlaka, Mashirika na Makampuni. Taasisi hizo ni kama ifuatavyo:
- Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA);
- Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA);
- Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA);
- Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL);
- Shirika la Reli Tanzania (TRC);
- Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO);
- Kampuni ya Meli ya Tanzania na China (SINOTASHIP).
VYUO VYA MAFUNZO
Wizara ya Uchukuzi inasimamia Vyuo viwili (2) vinavyotoa mafunzo ya usafiri na usafirishaji ikiwa ni pamoja na mafunzo ya matengenezo ya vyombo vya usafiri hususani katika usafiri kwa njia ya Anga. kama ifuatavyo:
- Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT);
- Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) ;
VYUO VYA MAFUNZO VILIVYOCHINI YA USIMAMIZI WA TAASISI
Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi zinasimamia vyuo vinne (4) vinavyotoa mafunzo ya uchukuzi na hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafunzo ya wataalam katika ngazi ya fundi mchundo kama ifuatavyo : -
- Chuo cha Hali ya Hewa, Kigoma
- Chuo cha Reli, Tabora
- Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), Dar es Salaam
- Chuo cha Bandari Dar es Salaam.
MABARAZA YA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI
Mabaraza ya Watumiaji wa Huduma za Usafiri yanayofanya kazi kwa kushirikiana na Mamlaka za Udhibiti ni:-
- Baraza la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC); na
- Baraza la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA - CCC).