KAMATI MIUNDOMBONU YATAKA MUARUBAINI FOLENI DAR ES SALAAM
KAMATI MIUNDOMBONU YATAKA MUARUBAINI FOLENI DAR ES SALAAM
Imewekwa: 19 Aug, 2026
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu imeitaka Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kushugulikia changamoto ya msongamano wa shehena ya mizigo bandarini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Selemani Kakoso amesema kuwa ni kweli bandari inafanya vizuri lakini kusongamana kwa mizigo na kuchelewa kutoka kunasababisha changamoto kubwa kwa watumiaji.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema kuwa msongamano huo unatokana na maboresho yaliyofanyika na kuwavutia wafanyabiashara kutumia bandari hiyo huku akiahidi kufanyia kazi changamoto iliyopo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya reli.
