Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa afungua Mkutano wa 17 wa tathmini ya Utendaji wa Wizara ya Uchukuzi

Imewekwa: 31 Oct, 2024
Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa afungua Mkutano wa 17 wa tathmini ya Utendaji wa Wizara ya Uchukuzi

Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amefungua Mkutano wa 17 wa tathmini ya Utendaji wa Wizara ya Uchukuzi unaofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha(AICC).

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Prof Mbarawa amesema Serikali imehuisha sera mbali mbali za uchukuzi ikiwemo sheria namba 10 ya reli ya mwaka 2017 ambapo sasa inaruhusu watoa huduma binafsi kununua vichwa na mabehewa na kutumia njia ya reli kwa kulipia tozo na kuwaasa wadau kuendelea kutoa maoni ili kuboresha zaidi na kuchochea uchumi wa nchi.