Waziri Mkuu wa DRC, Mhe. Bi. Judith Suminwa Tuluka, atembelea Bandari Kavu ya Kwala Mkoani Pwani,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Bi. Judith Suminwa Tuluka, leo Novemba 3, 2026, ametembelea Bandari Kavu ya Kwala Mkoani Pwani, akiwa ameambatana na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Katika ziara hiyo, viongozi hao walisafiri kwa treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Stesheni ya Magufuli Jijini Dar es Salaam mpaka Kwala. Akiwa ndani ya treni, Mhe. Judith, alielezwa kuhusu ushirikiano kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari Kavu ya Kwala.
Aidha ameelezwa kuwa ushirikiano huo unalenga kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kupunguza msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia matumizi ya usafiri wa reli.
Wakurugenzi wakuu wa Mashirika ya Reli Tanzania ( TRC) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Machibya Shiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, walikuwepo katika msafara huo.
