Waziri Mkuu Majaliwa asisitiza Weledi utekeleaji Mradi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhakikisha wataalam watakaopata fursa ya kushiriki katika mradi wa System Observation Financing Facility (SOFF) wanafanya kazi kwa weledi na maarifa ili kuuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati na viwango.
Akizungumza jijini Dodoma 21 Januari 2025 mara baada uzinduzi wa mradi huo Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kuwa kukamilika kwa wakati kwa mradi huo kwa wakati kutaimarisha utoaji wa taarifa za hali ya Hewa Nchini na kuwawezesha wadau wote kutumia taarifa katika mipango ya maendeleo.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa ameeleza umuhimu wa mradi huo kwa Taifa na kuzitaka Mamlaka zote kujiandaa kwa utekelezaji wa mradi hususani kwa maeneo yatakayoainishwa kwa utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake Naibu Waziri Wa Uchukuzi Mheshimiwa David Kihenzile Serikali imeeendelea kuiwezesha TMA kwa utekelezaji wa Miradi na Uwekezaji wa Rasilimali mazingira yanayosababisha wataalam wa TMA kushika Nyadhifa mbalimbali katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO).
Naye Kaimu Mkurugenzi wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika Miundombinu ya Hali ya Hewa Hali iliyoongeza usahiji wa taarifa kufikia asilimia 90.
Mradi wa SOFF utagharimu ni Dola za Marekani Milioni 13.9 ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoa Dola za Marekani Milioni 4.8 kwa kutoa ardhi ambapo vituo vitajengwa na rasilimali watu zinazohitajika. Aidha, mradi huo utahusisha miundombinu ya hali ya hewa inayohitajika ya GBON ambayo kwa Tanzania ni vituo 27 vya uangazi wa usawa wa ardhi na vituo vitano (5) vya uangazi wa angani na kuendeleza ujuzi wa wataalamu na taasisi kuendesha na kuendeleza mtandao wa uangalizi ili kukidhi mahitaji ya GBON.
Pia kati ya vituo 27 vya uangalizi wa ardhi vinavyohitajika, mradi wa SOFF utasaidia ununuzi wa vituo vipya tisa (9) na kuboresha vituo 18 vya uangazi vya usawa wa ardhi.