Waziri Prof. Mbarawa Aridhishwa na Mradi CATC
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu mipya ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinachojengwa Banana, Dar es Salaam, na kueleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo.
Mhe. Waziri Mbarawa alipokewa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri Bakari, ambaye alimhakikishia Mhe Waziri kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati, Dkt .Bakari aliambatana pamoja na Menejimenti ya TCAA.
Akizungumzia baada ya kutembelea mradi huo jijini Dar es Salaam, 23 Julai 2026, Mhe. Waziri Mbarawa alisema mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 23.9 ya utekelezaji ikiwa ni miezi 11 tangu kuanza kwa mradi.
Mradi huo wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 78 unalenga kuwezesha upatikanaji wa miundombinu ya kisasa ya mafunzo ya usafiri wa anga na kuimarisha nafasi ya Tanzania kuwa kitovu cha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
