WAZIRI MBARAWA AFUNGUA HOTELI UNGUJA

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi inaendelea kuwekeza wawekezaji katika sekta mbalimbali hasa sekta ya Hotel na Utali.
Mbarawa ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mradi wa Hoteli ya Palumbo Mnemba view iliyopo Matemwe Mkoani Kaskazini Unguja.
“Utaona jinsi gani wawekezaji wa hoteli hii wameweza kushirikiana na kuwekeza katika mradi wenye hadhi ya juu wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 14 na unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 80 kwa wananchi wa Zanzibar.” Alisema Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Unguja kuwa manufaa ya Miradi mradi huo yatakusa jamii na Serikali kwa ujumla sababu mradi huo umewekezwa kwa mashirikiano baina ya Mwekezaji Mzalendo kwa hisa za asilimia 80 na mwekezaji mgeni kutoka nchini Italia kwa hisa za asilimia 20.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Shariff A. Shariff amesema kuwa uwekezaji huo umekuza ajira pia umeongeza fedha za Kigeni hivyo kutoa wito kwa wakezaji mbalimbali kuwekeza Zanzibar.
Naye mmiliki wa hoteli hiyo Pablo PDS. Palumbo ameishukuru serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari kwa ushirikiano uliompa katika kuhakikisha ameekeza katika ujenzi wa hoteli hiyo ambayo ina vyumba themanini (80) na lengo kuwa na vyuma miamoja.
Ufunguzi wa hoteli hiyo ni moja ya shamra shamra ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 61 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibari.