TANZANIA YAONGOZA KIKAO CHA 10 CHA MOESNA, WAZIRI MKUU AZINDUA MTAALA WA MAFUNZO YA WAENDESHA VYOMBO KWA NJIA YA MAJI
Tanzania imeongoza Kikao cha 10 cha Jumuiya ya Maritime Organization for Eastern, Southern and Northern Africa (MOESNA), kilichofanyika Oktoba 15, 2026, jijini Dar es Salaam, kikihudhuriwa na Mawaziri 26 wanaosimamia sekta ya uchukuzi na lojistiki pamoja na wajumbe kutoka nchi wanachama,Kikao ambacho kimelenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika maendeleo ya sekta ya usafiri majini
Akifungua kikao hicho, Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameipongeza Wizara ya Uchukuzi na wadau wake kwa maandalizi, akieleza kuwa ushirikiano wa kikanda ni muhimu katika kukuza uchumi na kuboresha huduma za usafiri majini, akisema nafasi ya kimkakati ya Tanzania inaifanya nchi kuwa lango muhimu la biashara na usafirishaji linalounganisha mataifa ya Afrika na masoko ya kimataifa
Akizungumzia miundombinu ya usafirishaji, Dkt. Nchemba amesisitiza umuhimu wa kuunganisha usafiri wa majini na njia nyingine za usafirishaji ili kuongeza ufanisi na kupanua fursa za biashara, akibainisha juhudi za Serikali za kuifufua reli ya TAZARA zitasaidia kuimarisha uhusiano wa usafiri kati ya Tanzania na Zambia, na kuchochea ukuaji wa uchumi
Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi na Mwenyekiti wa MOESNA, Prof. Makame Mbarawa, amesema Tanzania itaelekeza nguvu katika kuimarisha usafiri wa majini, kuongeza fursa za mafunzo na kujenga uwezo wa wataalamu na washirika hatua ambazo zitawezesha kubadilishana ujuzi na uzoefu miongoni mwa nchi wanachama, sambamba na kuboresha usalama, ufanisi na ushindani wa sekta hiyo katika ukanda wa MOESNA
Katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa MOESNA, Bw. Kassim Mpaata, aliwasilisha programu kuu za taasisi hiyo kwa ajili ya kujadiliwa na wajumbe, Aidha, Botswana, Burundi, Malawi na Sudan Kusini zilitambuliwa rasmi kama nchi wanachama wapya, hatua inayodhihirisha kupanuka kwa ushiriki na ushirikiano wa kikanda kupitia MOESNA
Hatua nyingine muhimu ilikuwa uzinduzi wa Regional Coxswain Training Curriculum uliofanywa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba,Mtaala ambao unalenga kuimarisha mafunzo ya waendesha vyombo vya maji.
