SHIRIKA LA NDEGE LA BRUSSELS KUTOKA UBELGIJI YAANDA SAFARI ZA KUJA TANZANIA
Shirika la ndege la Brussels (Brussels Airlines) kutoka Brussels nchini Ubeligiji imeandika historia mpya Nchini Tanzania hasa katika Sekta ya Usafiri wa Anga, Utalii na Biashara baada ya Shirika hilo kuzindua rasmi safari zake za mojakwamoja kati ya Brussels ,Ubelgiji kuja Tanzania kupita uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hafla ya mapokezi yao imefanyika tarehe Juni 3 ,2026.
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa aliongoza viongozi mbalimbali kuipokea ndege hiyo amesema kuwa kuanza kwa safari hiyo ni kufungua fursa za kiutalii , biashara na mahusino kwa nchi mbili kati Tanzania na Ubelgiji, pia aliongeza kusema kuwa haya yote yanafanyika kutoka na mazingira mazuri yaliyotengenezwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan.
Pia Mbarawa amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini hususani kiwanja cha ndege cha KIA kwa kujenga jengo la Kisasa la Abiria ili kundelea kuvutia mashirika mengine ya ndege kuja Tanzania.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. James Millya (Mb), amesema uzinduzi wa Safari hizo kutoka Brussels, makao makuu ya umoja wa Ulaya (EU) nia ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Ubelgiji pamoja na nchi nyingine za Ulaya.
Naye Rais wa Shirika hilo Julia Hilenbrand amesema kuwa kuanza kwa safari hizo ni hatua muhimu katika Safari za Anga kati ya Tanzania na Ubelgiji kwa kwa sasa watalii na wafanyabiashara watatoka Ubelgiji na kuja Tanzania.
Huku Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Abdul Mombokaleo amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini ili mashirika mengi ya ndege yaweze kuja nchini Tanzania.
