Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Serikali kujenga gati 5 Bandari ya Dar es Salaam

Imewekwa: 04 Jun, 2024
Serikali kujenga gati  5 Bandari ya Dar es Salaam

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema inakusudia kuongeza ukubwa wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kujenga gati mpya tano zenye urefu wa mita 300

Kauli hiyo ya Serikali  imetolewa leo tarehe 3 June 2024 na Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Uchukuzi  Dkt.Ally Possi alipofanya ziara katika Bandari ya Dar-es-Salaam ili kujionea mwenendo wa kazi.

Dkt.Possi amesema eneo la Bandari ni dogo na kwahivyo Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza eneo la bandari ili kupata gati za kuhudumia meli nyingi zaidi na lengo likiwa ni kuifanya iwe 'hub' ya shughuli za kibandari katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA,Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bwa.Mrisho S.Mrisho amesema mpaka kufikia Aprili mwaka huu,Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa imehudumia  tani milioni 19.6 kiasi ambacho kinakaribia kuvuka lengo la kuhudumia tani milioni 22.