PROF. GODIUS KAHYARARA AHIMIZA WADAU KUTUMIA BANDARI KAVU YA KWALA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Khayarara amewataka wadau wa Bandari ya Dar es Salaam kuongeza kasi ya kutumia Bandari kavu ya Kwala ili kuondoa Msongamano na Foleni katika Jiji la Dar es salaam.
Prof. Kahyarara ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika kikao kilichowakutanisha wadau wa bandari kutoka TRA,TBS, TATOA, TRC,TAZARA,TASAC,TMA na Wizara ya Uchukuzi.
“Bandari Kavu ya Kwala imeshanduliwa na imeanza kufanya na hivyo niwasisitize muitumie kwa kupeleka mizigo ikiwemo makasha na magari ili kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam” amesema Prof. Kahyarara.
Katibu Mkuu Prof. Kahyarara ametumia Mkutano huo kuwaka TRC kuhakikisha wanakuwa na vichwa vya kutosha ili kuweza kuhudumia makasha na mizigo mingine.
Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Abedi Gallus amesema kuwa TPA imeongezewa hekali 42 eneo la Kurasini kwa ajili ya kutoa huduma ya Mizigo na Maroli Hali itakayoongeza kasi ya uondoshaji wa mizigo ndani ya Bandari.
Naye Mkurugunzi wa Miundombinu kutoka wizara uchukuzi Shomari Shomari ameweka wazi sababu zinazosababisha msongamano jijini Dar es Salaam kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara,Utumiaji Mbovu wa Barabara na Madereva kutofuta Sheria na kusema kuwa kuanza kutumika kwa Bandari Kavu ya Kwala kutakuwa muarobaini wa changamoto ya msongamano hususani katika Barabara na Bandarini.
Kikao cha Maboresho ya Bandari haufanyi ma kila mwezi huku lengo likiwa kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabli wadau wa Bandari.