NAIBU WAZIRI KIHENZILE ASISITIZA WAHANDISI WA NDANI KUJIFUNZA

Serikali imeeleza faida za Wahandisi wa ndani kushiriki kikamilifu kwenye Miradi ya Miundombinu inayoendelea kujengwa nchini kuwa ni pamoja na kusaidia kupunguza gharama kwa Usimamizi na Ujenzi wa Miradi kama hiy itakapoanza kutekelezwa kwenye maeneo mengine Nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam 23 Januari 2025 mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa sehemu ya reli ya Kisasa ya SGR inayoelekea Bandarini Naibu Waziri Wa Uchukuzi David Kihenzile amesema wataalam wazazi walioshiriki kwenye Ujenzi huo wana wajibu wa kuhakikisha wanabaki na utaalam huo.
Naibu Waziri Kihenzile ametumia fursa hiyo kuwapongeza wahandisi wazawa pamoja Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuendelea kusimamia mradi huo ambao kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 85.