Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Naibu Waziri Kihenzile amuwakilisha Waziri Wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa kufungua Mkutano Mkuu (TASAA)

Imewekwa: 02 Mar, 2026
Naibu Waziri  Kihenzile amuwakilisha Waziri Wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa kufungua Mkutano Mkuu  (TASAA)

Naibu Waziri Wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amuwakilisha Waziri Wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa kufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa  Mawakala Forodha Tanzania (TASAA) 27 Februari 2026 jijini Dar es Salaam

Kupitia Jukwa Naibu Waziri Kihenzile amewaeleza wadau hao kazi inayofanywa na Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uboreshaji wa Miundombinu ya Uchukuzi ikiwemo Badari, Meli, Reli, Viwanja Vya Ndege kazi ambayo imeanza kuwa na matokeo makubwa kwenye mnyororo wa Uchumi wa Nchi.

Naibu Waziri Kihenzile amepokea tuzo na cheti maalum kilichoandaliwa na Umoja cha kutambua mchango wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu katika uboreshaji wa Miundombinu ya Uchukuzi Nchini.