Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

MV MWANZA YAANZA SAFARI KWENDA BUKOBA

Imewekwa: 09 Oct, 2025
MV MWANZA YAANZA SAFARI KWENDA BUKOBA

Meli ya MV Mwanza iliyoanza kutengenezwa mwaka 2019 yenye uwezo wa kubeba abiria 12000 na Mizigo tani 400 imekamilika na kuanza Safari kutoka Mwanza  kwenda Bukoba leo tarehe 07 Oktoba 2025.

Meli hiyo ya Kisasa imeandika historia Mpya katika Ziwa Victoria na kuwa ni meli ya Kwanza kubwa katika Ziwa hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Erasto Sima amesema kuwa kuanza kazi kwa Meli hiyo kutasaidia kurahisisha usafiri katika Ziwa Victoria na kuinua Uchumi katika Wilaya Bukoba na Kagera kwa Ujumla.

“Wafanyabishara na wananchi wengi walikuwa wanaisubiria Meli hii kwani ni mkumbozi katika kusafairisha mizigo na abiria na hata kusaidia kukuza sekta ya utalii, maana meli hii ni kubwa na imekuwa ni kivutio kwa kila anaeiona” Amesema Mhe. Sima

Kwa Upande Mkurugenzi Mtendaji wa TASHICO Erick Hamiss amesema kuwa katika safari hii ya kwanza meli hiyo imebeba abiria 400 pamoja na Mizigo zaidi ya tani 70, aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kiutumia meli hiyo kwani ni meli ya kisasa na inauwezo wa kubeba abilia 1200 na mizigo tani 400.

“Meli hii ya kisasa itakuwa inafanya Safari zake kati ya Mwanza, Kemondo, Bukoba mpaka Port bell nchini Uganda” Amesema Erick.

Mha. Saidi Kaheneko-Kaimu Meneja Msajiri wa Meli na Ukaguzi kutoka TASAC amesema kuwa TASAC imeridhishwa na utendaji wa meli hiyo katika safari hii kwani imefanyiwa maboresho yaliyoonekana wakati wa majaribio na kusisitiza kuwa Meli hiyo ina mifumo na vifaa vya kisasa na Shirika hilo limejiridhisha kuwa meli hiyo imekizi vigezo na kupatiwa cheti  kwa ajili ya kutoa huduma.