Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

MV. MBEYA II MKOMBOZI USAFIRI WA MAJINI KWA WANANCHI WA RUVUMA NA MBEYA

Imewekwa: 30 Oct, 2023
MV. MBEYA II MKOMBOZI USAFIRI WA MAJINI KWA WANANCHI WA RUVUMA NA MBEYA

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi David Kihenzile ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kupitia Kitengo cha Uhusiano kuhakikisha inaweka mikakati madhubuti ya kukitangaza Kiwanja cha Ndege cha Songwe ili kuruhusu mashirika mengi zaidi kukitumia.

 

Naibu Waziri Kihenzile ameyasema hayo mara baada kutembelea Kiwanja hicho Mkoani Mbeya na kusema kukamilika kwa mradi wa barabara ya kuruka na kutua ndege pamoja na taa ni fursa kwa abiria na wafanyabishara wanaozalisha mazao mbalimbali mkoani humo kwani wataweza kusafirisha bidhaa zao kwa usafiri wa ndege.

 

“Serikali imeshakamilisha mradi wa barabara ya kuruuka na kutua ndege pia tumeweka taa hapa hivyo hatuna sababu ya kukosa mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi kuja hapa sababu kiwanja kinatoa huduma kwa saa 24’ amesema Naibu Waziri Kihenzile.

 

Naibu Waziri Kihenzile ameitaka TAA kuhakikihisha inajenga jengo maalum (COLDROOM) litakalotumika kuhifadhi mazao ili kuruhusu mzigo mkubwa zaidi wa mazao kusafirishwa kupitia kiwanja hicho hasa ukizngatia mkoa wa Mbeya na mikoa jirani inazalishwa mazao ya matunda ikiwemo parachichi.

 

Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amezitaka taasisi zinazosimamia ujengo wa jengo jipya la abiria kumsimamia kwa karibu Mkandarasi ili kuhakikisha anakamilisha kazi zilizobaki za ujenzi wa jengo hilo.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa amesema kwa sasa uongozi wa Mkoa umeanza kuwahamasisha wakulima wa mboga mboga na mazao mkoani kuongeza uzalishaji ili kuweza kuuza mazao hayo ndani nan je yan chi na kuinua pato.

 

Naye Meneja wa Kiwanja cha Ndehe cha Songwe Pascal Kalumbeta amesema kwa sasa KIwanja hicho kinahudumia mashirika mawili ya ndege ikiwemo Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Precision ambayo yanatoa huduma kwa ratiba.

 

Naibu Waziri Kihenzile yuko katika ziara ya siku nne Mkoani Mbeya ya kukagua miundombinu ya reli, viwanja vya ndege,meli na Bandari.