Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

MRADI WA MATENKI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA MAFUTA NCHINI-PROF. MBARAWA

Imewekwa: 13 Sep, 2024
MRADI WA MATENKI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA MAFUTA NCHINI-PROF. MBARAWA

Waziri wa Uchukuzi  Profesa  Makame mbarawa ametembelea  ujenzi wa matenki ya mafuta unaondelea jijini Dar es salaam maeneo ya Tungi kigamboni ambapo amesema kuwa  matenki hayo yatakuwa 14 huku matenki sita yatakuwa ya dizeli na 5 yakiwa ni ya petrol.

 

Akizungumza Jijini  Dar es salam  Mara  baada ya kutembelea ujenzi huo Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huu utagarimu kiasi cha Fedha  shilingi Bilioni 678 na utaenda kuleta manufaa makubwa kwenye nchi yetu kwani mara baada ya kumalizika mradi huo tutapunguza changamoto za Mafuta.

 

"Tunafahamu  kuwa kwa sasa meli za mafuta zinachukua muda mrefu. Katika kuleta mafuta hii inatokana. Na upungufu wa matenki yaliyopo nchini pia  mafuta hayo yakitolewa yanapelekwa kwenye  vituo husika  na sisi kama serikali tumeamua kujenga mantenki ili yawekewe mafuta  na kupelekea wateja wetu.

 

 

Aidha  ameongeza kuwa mradi huu unaenda kutekelezwa Kwa Miaka 2 Miwili kutokana na hali za Mvua pia Mamlaka ya usimamizi wa bandari (TPA) kwa kushirikiana  na wakandarasi

Watasimamia ujenzi huo mpaka kukamilika na kuweza kukabidhi Rasmi.

 

Natoa  wito kwa wasimamizi  wote ambao  wamepewa kusimamia ujenzi huo kufanya kazi vyema na uwe mradi bora zaidi kwani serikali kupitia Dkt samia suluhu hassani ametoa fedha za kutosha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wa mantenki.

 

Kwa upande  wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari (TPA)  Juma  Kijavala amesema kuwa Mradi huo unaenda kutekelezwa kwa wakati ili huduma za mafuta ziweze kuendelea  nchini.

 

Naye Meneja  wa  Mardi huo. Mhandisi Hamisi  Hassani amesema kuwa  manteki  hayo ya mafuta  yatakuwa na  ujazo wa 27  kwa Tenki moja la dizeli huku oil ikiwa ni 27 hivyo jumla ya ujazo itakuwa ni 378 pia mradi huu unaenda kupunguza kero  ya  mafuta ikiwemo bandarini na nitahakikisha mradi huu unaenda kuisha kwa wakati ambapo umepangwa.

 

Vilevile  Mstahiki  Meya kutoka kigamboni na diwani wa kata ya Tungi  Ernest Mafimbo   ametoa pongezi kwa Serikali kwa kuweza kupeleka mradi huo kigamboni kwani itaenda kupelekea Ajira hususani kwa Vijana, Mama lishe  pia sisi kama manispaa ya kigamboni tunaenda kupata manufaa kupitia mradi huo.