Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Miradi ya Meli Ziwa Tanganyika kuchagiza Uchumi

Imewekwa: 19 Aug, 2025
Miradi ya Meli Ziwa Tanganyika kuchagiza Uchumi

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluh Hassani imedhamiri kufungua mkoa wa kigoma kwa kujenga na kukarabati meli ambazo zitakazopokamilika zitakuza uchumi wa wananchi wa Mkoa huo pamoja na Nchi jirani zinazozunguka Ziwa Tanganyika.

Hayo yamesemwa na Naibu  Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile wakati alipotembelea na kukagua mradi wa Meli ya MV Liemba,MV Muongozo pamoja na Kiwanda cha kujenga na kukarabati Meli.

Aidha  Naibu Waziri Kihenzile amesema kuwa meli ya MV Liemba, ni meli ya kihistoria iliyojengwa mwaka 1913, na iliharibika  mwaka  2018 ambapo kwasasa Ukarabati wake, umefikia 25%, na kukamilika kwake kutaiwezesha kubeba  abiria 600 na mizigo tani 200.

Aidha, meli ya MV Mwongozo, yenye uwezo sawa wa kubeba abiria na tani 80 za mizigo, Serikali iko katika hatua za mwisho ili kufanya malipo ya awali kwa Mkandarasi. Wakati huo huo, MT Sangara — meli ya mafuta yenye uwezo wa kubeba lita 410,000 — inaendelea kutoa huduma kwasasa kwa upande wa Kigoma na nchi jirani ya Congo.

Katika hatua nyengine Naibu waziri ametembela ujenzi wa kiwanda kipya cha ujenzi na ukarabati wa meli, ambapo amesema kuwa mradi wa ujenzi  wa kiwanda hicho utakapo kamilika  kitakuwa na uwezo kujenga meli mbili zenye ujazo wa tani 5000 kwa wakati mmoja  na hivyo kuwa kitovu cha maendeleo ya usafirisha katika ziwa Tanganyika.