Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YAPONGWEZWA UENDESHAJI

Imewekwa: 24 Oct, 2023
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YAPONGWEZWA UENDESHAJI

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile ameipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kuendelea kusimamia na kuendesha viwanja vya ndege kwa weleldi hali iliyoongeza idadi ya mashirika ya ndege ya ndani na nje katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza mara baada ya kuzungumza na Menejimenti ya TAA, Naibu Waziri Kihenzile amesema usimamizi huo uimarishwe kwenye miradi ya maendeleo inayofanywa na TAA ili ikamlike kwa wakati na viwango.

 

“Hongereni kwa kazi nzuri mnayoifanya hasa kwenye usimamizi wa viwanja vya ndege mnavyovisimamia nguvu hii inapaswa kuwekwa pia kwenye miradi inayoendelea, ili ikamilike kwa wakati na tuone thamani ya fedha’ amesema Naibu Waziri Kihenzile.

 

Naibu Waziri Kihenzile ameitaka TAA kuhakikisha Viwanja vya Ndege vya Arusha na Iringa vinawekwa taa ili kuviwezesha kutumika saa 24 na kukuza uchumi wa kanda hizo.

 

Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa vibarua wanaofanya kazi kwenye miradi inayotekelezwa na taasisi za Uchukuzi hususani ujenzi wa miundombinu wanalipwa kwa wakati na kwa viwango wanavyokubalina ili kupunguza malalamiko kwenye utekezaji wa miraid hiyo..

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA Mussa Mbura amemuhakikishia Naibu Waziri Kihenzile kuwa TAA itahakikisha inaongeza nguvu kwenye usimamizi ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana na miradi inakamilika kwa wakati kulingana na mikataba.

 

Mkurugenzi Mbura ameongeza kuwa kwa sasa kupitia kiwanja cha Ndege cha JNIA safari za ndege zimeendelea kuongezeka kwa asilimia 29, abiria asilimia 50 na tani za mizigo zimeongezeka kwa asilimia 15.

 

Naibu Waziri Kihenzile yuko katika ziara ya siku 5 jijini Dar es Salaam ya kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi hizo pamoja na kuzungumza na menejimenti za taasisi hizo.