Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE TABORA

Imewekwa: 10 Oct, 2024
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE TABORA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango ameipongeza Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Ujenzi kwa kusimamia vema mradi wa ujenzi wa jengo la abiria katika kiwanja cha ndege Tabora. 

Dr. Mpango ametoa pongezi hizo leo wakati aliweka jiwe la msingi katika jengo la abiria linaloendelea kujengwa katika kiwanja cha ndege Tabora. 

"Macho yangu yananiambia kuwa hapa tutapata jengo zuri kabisa, hakika ni jambo la kutia moyo kwamba fedha za wananchi zinatumika sawasawa na ilivyopangwa," Amesema Dr.Mpango.

Awali akizungumza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mhandisi Mohamed Besta,amesema mradi huo wa ujenzi umefikia asilimia 72, huku akibainisha kuwa jengo hilo linatarajiwa kuwa na sakafu ya chini na ya juu.

Besta amesema kuwa katika sakafu ya chini jengo  hilo linatarajiwa kuwa na ofisi za kampuni mbalimbali za ndege kwa ajili ya tiketi pamoja na eneo maalum la kupumzikia abiria. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania  Abdul Mombokaleo ameishukuru serikali kwa jitihada zake katika kuboresha usafiri wa anga uku akiahidi kuwekwa kwa mikakati bora ya kibiashara ambayo itakifanya kiwanja hicho kuwa na matokeo yaliyokisudiwa.