Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

KFC YATAKIWA KUFUNGUA MGAHAWA KATIKA STESHENI YA SGR DODOMA

Imewekwa: 12 Feb, 2025
KFC YATAKIWA KUFUNGUA MGAHAWA KATIKA STESHENI YA SGR DODOMA

Prof. Mbarawa amesema KFC imetoa fursa ya ajira mpya kwa vijana wa kitanzania, vilevile kampuni hutoa mafunzo kwa watanzania zaidia ya 800 ikiwapa ujuzi muhimu ikiwemo ukarimu, huduma ya chakula na usalama wa chakula na usimamizi bora wa chakula.

"Uwepo wa KFC katika maeneo muhimu ya usafiri kama SGR unaimairisha shughuli za kiuchumi kwa kutoa ajira thabiti na fursa za kujenga ujuzi hivyo nawaelekeza mfunguwe mgahawa kama huu katika Stesheni ya Dodoma " ameongeza .Prof. Mbarawa.

Aidha Prof  Mbarawa ameongeza kua KFC inafanya shughuli za uhamasishaji wa bidhaa za ndani na ukuaji wa kiuchumi kwani imejitolea kuendesha mipango ya kuhamasisha matumizi ya malighafi na vifaa vya ndani ili kuunga mkono wasambazaji wa Tanzania na kupunguza utegemezi wa uagizaji nje ya nchi.

"Ushirikiano wa ndani unachangia katika sekta za kilimo na viwanda vya Tanzania na hii inaweka chachu katika kukuza fursa zaidia za ajira ya moja kwa moja" amesisitiza. Mbarawa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Edward Mpogolo ameipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa ushirikiano mkubwa inaowapa wafanyabiashara na wawekezaji wanaowekeza katika stesheni za SGR kwani inachangia kukuza uchumi na kutoa ajira kwa vijana nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli - TRC Ndugu Masanja amesema kua majengo ya stesheni za SGR yamezingatia utoaji wa huduma za kijamii kwa abiria ikiwemo migahawa ,maduka makubwa na maduka madogo madogo kupitia wawekezaji wanaowekeza katika stesheni.

Mkurugenzi Mkuu wa Dough Works Limited Ndugu Vikram Desai amesema ufunguzi wa KFC katika stesheni ya SGR ya Magufuli ni alama ya ukuaji wa haraka wa miundombinu nchini Tanzania na ni jukumu muhimu katika sekta binafsi katika ukuaji wa taifa kiuchumi.

"SGR imeleta mabadiliko katika biashara, usafiri na fursa za kiuchumi hivyo na sisi KFC tunajivunia kuhudumia jamii ya kitanzania na wasafiri wa SGR" ameongeza Mkurugenzi Vikram.

Wizara ya Uchukuzi inaendelea kuunga mkono juhudi za kuendeleza na kuboresha miundombinu na huduma za usafirishaji kwa manufaa ya nchi na nchi jirani.