Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Katibu Mkuu Prof. Kahyarara akutana na wadau wa Usafirishaji jijini Dar es Salaam

Imewekwa: 22 May, 2024
Katibu Mkuu Prof. Kahyarara akutana na wadau wa Usafirishaji jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof Godius Kahyarara leo Tarehe 21 Mei,2024 ameongoza Mkutano wa Mashauriano na wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji nchini kuhusu hatua za kuchukua ili kupunguza ongezeko la viwango vya usafirishaji wa mizigo baharini uliofanyika kwenye ofisi za Latla Jijini Dar es salaam

 

Prof Kahyarara amewashukuru wadau wa usafirishaji Kwa njia ya maji Kwa kujitokeza Kwa wingi ili kujadili Kwa pamoja masuala yanayowahusu kwa manufaa ya Sekta ya Usafirishaji Kwa njia ya maji Nchini

 

"Tumieni fursa hii tujadiliane Kwa uwazi changamoto zetu zote tunazokumbana nazo katika Usafirishaji Kwa njia ya maji na tupendekeze njia mbadala za kupunguza au kuzimaliza kabisa na nawahakikishia masuala yote yatakayokuwa kwenye uwezo wetu kama Wizara ya Uchukuzi tutayafanyia kazi haraka" amesisitiza Kahyarara

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) Bw. Mohamed Salum amesema  mikutano ya wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji nchini ni muhimu sana kwani inasaidia kujenga uelewa wa pamoja ambao utainua na kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji wa mizigo kwa njia ya maji ambavyo vitasaidia uimarishaji wa huduma kwa wananchi kwa manufaa ya Taifa