Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

KAMATI YASISITIZA UFANISI KWENYE UCHUKUZI

Imewekwa: 22 Jan, 2026
KAMATI YASISITIZA UFANISI KWENYE UCHUKUZI

Kamati ya Bunge ya miundombinu imeitaka Wizara ya Uchukuzi kuboresha maeneo mbalimbali yenye udhaifu katika taasisi zake ili kuleta ufanisi unaotarajiwa na wananchi katika sekta hiyo.

Hayo yameelezwa leo bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso, katika kikao cha kamati hiyo na Viongozi kutoka Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake nne ambazo ni Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA), Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Ndege (ATCL) .

Kakoso amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya usafirishaji tofauti na miaka kadhaa iliyopita, japo bado yapo maeneo mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi hivyo wizara inapaswa kusimamia kazi ya kuboresha maeneo yaliyosalia.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa wizara itafanyia kazi maoni yaliyotolewa na kamati na kuahidi kuwasilisha baadhi ya majibuya maswali ya wajumbe kwa maandishi ili kuleta uelewa zaidi kwa wajumbe.

Aidha Mbarawa amesema kuwa utaratibu kwa ajili ya ziara ya kujifunza kwa wajumbe juu ya namna taasisi zilizo chini ya wizara zinavyofanya kazi unaandaliwa, huku akiwahakikishia wajumbe kuwa baada ya ziara hiyo watakuwa wajumbe wazuri kwa wananchi juu ya utendaji wa serikali.