KAMATI YA SGR YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA SGR KUANZA SAFARI ZA DAR ES SALAAM MPAKA MOROGORO
Kamati ya usimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara leo wamekagua ujenzi wa kipande cha Reli kutoka Dar es Salaam Mpaka Morogoro na kuridhika na maandalizi yaliyofanywa ya kuanza safari zake kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro 14 Juni 2024.
Kahyarara amesema kuwa Maandalizi ya kuanza safari hiyo kwa kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro yapo tayari na kutoa wito kwa wananchi kutumia usafiri huo mara watakapoanza.
“ Maandalizi ya safari yamekamalika na Juni 14,2024 itaanza safari kutoka Dar es salaam mpaka Morogororo yamekarika na kila kitu kipo sawa” Alisema Kahyrara.
Lawrence Mafuru ni katibu Mtendaji Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa anasema kuwa Kutarajia kuanza kwa safari ya Treni hiyo kutasidia kuinua uchumi wa Nchi pia kurahisisha usafirishaji wa Abiria na Mizigo hivyo tutaongeza mapato ya nchi.
Reli ya SGR ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu pia na nchi jirani kuweza kutumia reli yetu.
Huku mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa vivuko kwa watembea kwa miguu na vivuko vya Magari vinatarajia kukamilika juni 10 Mwaka huu.