Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

Kamati ya Miundombonu yasisitiza mifumo kuungana

Imewekwa: 20 Oct, 2026
Kamati ya Miundombonu yasisitiza mifumo kuungana

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Wizara ya Uchukuzi kupitia Mamlaka ya Usafiri Ardhini (Latra) kuhakikisha mifumo ya Latra, Serikali Mtandao (Ega) na Polisi inasomana ili kuepuka changamoto na mvutano na wadau wa sekta ya usafiri nchini.

Hayo yameelezwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso katika kikao kilichofanyika bungeni Dodoma ambapo Latra wamewasilisha taarifa ya maboresho ya Mfumo wa kudhibiti Mwendokasi (VTS).

Kakoso amesisitiza umuhimu wa serikali kushughulikia malalamiko ya wadau wa usafiri na kutafuta suluhu kwenye kila changamoto inayojitokeza.

Aidha Kakoso ameongeza kuwa ni muhimu kuhakikisha wadau wanashirikishwa na kupata taarifa juu ya mabadiriko yoyote yanayotarajiwa kufanyika kwani wao ndiyo watekelezaji wa mabadiliko hayo.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameishukuru kamati kwa kuishauri vyema serikali wakati wote na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na maoni kutoka kamati hiyo.