KAMATI YA KUDUMU YABUNGE YA MIUNDOMBINU YAPONGEZA WIZARA YA UCHUKUZI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Sulemani Kakoso ameipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kusimamia utekelezaji wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Kakoso amesema hayo kwenye kikao cha kupitisha na kujadili bajeti mwaka 2024/2025 ya wizara ya Uchukuzi kilichofanyika jijini Dodoma.
“ Nawapongeza sana kwa uwekezaji kwenye Bandari , Uwekezaji kwenye Reli ya SGR na tunaapongeza kutokana na huduma zinazotelewa na taasisi hizo pamoja na usimamizi mzuri unaofanya”
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema kuwa Serikali inaendelea na kuboresha huduma za Anga, Ujenzi wa Bandari n, ujenzi wa Meli na Ujenzi wa viwanja vya Ndege.
“Serikali inaendela kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali iliyopo chini ya Uchukuzi kama vile Ujenzi wa Meli, Upanuzi wa Bandari , Ujenzi wa Meli na Maboresho wa Viwanja vya Ndege” Alisema Kihenzile.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema kuwa kazi kubwa imefanywa na Serikali katika kuboresha miundombinu mbalimbali na kuendelea na ujenzi wa SGR, Ujenzi wa Viwanja vya Ndege na Ujenzi wa Meli katika Maziwa na Tanganyika, Nyasa na Victoria.