KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAPITISHA RANDAMA YA BAJETI WIZARA YA UCHUKUZI YA MWAKA 2026/2027.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepitisha Randama ya Mpango na Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na utekelezaji wa Maendeleo ya miradi kwa Mwaka wa fedha 2026 /2027 ya Wizara ya Uchukuzi hatua inayoelezea kuwa ni uboreshaji na utekelezaji wa Miradi katika Sekta ya Uchukuzi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Selemani Kakoso ameipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kubaoresha miundombinu ya Bandari , Reli ,Anga na Uboreshaji wa Vyuo kama vile NIT na DMI,
“Mheshimiwa Mbarawa hongera sana, Kamati hii inawapongeza watumishi wote wa uchukuzi kwa kusimamia miradi ambayo manufaa yake yanaonekana tena yanatija kwa taifa letu mfano Upanuzi na ujenzi wa Bandari, ununuzi wa Vifaa vya kufunsishia katika chuo cha DMI na NIT pamoja na Usimamizi wa Shirika la ndege (ATCL)“ Alisema Mhe. Kakoso.
Katika hatua nyingine kamati hiyo imeipongeza wizara ya uchukuzi kupitia TPA kwa kubuni mradi wa ujenzi wa Matank ya Mafuta pia ujenzi na ubaoreshaji Wa bandari ya Tanga na Mtwara.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameishukuru kamati ya Miundombinu kwa kuidhinisha randama hiyo na kuahidi Wizara itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mairadi mbalimbali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vinavyokubalika .
Mbarawa amesema kuwa Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2026/2027 itaendelea na miradi ya Ujenzi wa SGR, upanuzi wa Bandari , ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya ndege na uboreshaji wa vyuo vya elimu vilivyo chini ya Wizara ya Uchukuzi.
