Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

CHANGAMOTO UHARAMIA KUTAFUTIWA UFUMBUZI-WAZIRI PROF. MBARAWA

Imewekwa: 29 Nov, 2024
CHANGAMOTO UHARAMIA KUTAFUTIWA UFUMBUZI-WAZIRI PROF. MBARAWA

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amebainisha kuwa changamoto ya uharamia iliyokuwepo katika eneo la bahari mwaka jana imeleta athari hususani katika usafirishaji wa mizigo.

 

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipofungua Mkutano wa Wataaalam wa masuala ya usafiri majini uliondaliwa kwa kushirikia na Shirika la Shirika la Bahari Duniani (IMO) na kusema kupitia Mkutano huo wataalam watachakata changamoto hizo na kutafuta muarobaini kwa pamoja.

 

‘Sote tunatambua changamoto zilitokea katika usafiri majini ikiwemo uharamua na kwa kutambua hilo Serikali zote hasa katika ukanda wa red sea, Guba ya Aaden, Djibouti zimekubaliana kwa pamoja  kuja na mikakati ya kupambana na changamoto hizo hii ni hatua ya kuunga mkono,” amesema Profesa Mbarawa.

 

Waziri Prof. Mbarawa amesema kuunganisha Nguvu kwa kutafuta Suluhu ya changamoto za usafiri Majini kwa pamoja kutaleta matokeo yatakayonufaisha Nchi zote zinazotegemea mzigo wake kupitia baharini.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani (IMO), Antonio Dominguez amesema usalama wa baharini una umuhimu mkubwa kwa uchumi wa dunia kwani unabeba ustawi wa mazingira na jamii kote ulimwenguni.

 

Amesema bila jitihada za pamoja katika kutokomeza changamoto za usafiri huo kutaongeza changamoto ya upatikanaji wa bidhaa, huduma na hata misaada ya kibinadamu ambayo ni muhimu kwa maisha ya mania watu duniani.

 

Katibu Mkuu Dominguez ameongeza kuwa asilimia 10 ya biashara ya kimataifa na takribani asilimia 22 ya kontena zote hupitja mfereji wa Suez Canal hivyo kukabiliana na changamoto kutachangia ongezeko la mzigo.