Bilioni 37 zatumika Kiwanja cha Ndege Songea
erikali imesema takriban sh. Bilioni 37 zimetumika kufanya ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Kiwanja cha ndege cha Songea hatua ambayo itachagiza kuongezeka kwa safari za ndege ambazo zitakidhi soko la wasafiri wa anga wa mkoa wa Ruvuma.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakati alipokagua kiwanja hicho na kusema maboresho hayo ni chachu itakayosaidia safari za ndege kufanyka kila siku za wiki.
“Kukamilika kwa uwanja wa ndege huu kumesababisha shirika letu la ndege kuanza safari zake za kawaida Air Tanzania sasa inakuja mara 3 kwa wiki tulitamani ije mara nyingi baadaa ya mara tatu labda tufanye ianze kufanya mara tano kwa wiki lakini baadae ianze kuja kila siku” Alisema Mbarawa.
Pamoja na hilo Waziri Mbarawa amesema kwa sasa wananchi wataendelea kutumia jengo dogo la abiria wakati Serikali inaendelea kufanya mchakato wa ujenzi wa jengo la kisasa la abiria ambalo litaweza kutoa huduma bora kwa wananchi ambazo zitaendana na hadhi ya kiwanja hiko.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameishukuru Serikali kwa kuimarisha sekta ya uchukuzi mkoani humo na kuendelea kutoa kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi iliyochini ya wizara hiyo.
Naye Meneja wa Kiwanja hicho Dustan Komba amesema maeneo yaliyoboresha ni pamoja na njia ya kutua na kurukia ndege na kutoka urefu wa mita 1600 kwenda mita 1860, usimikaji wa taa za kuongozea ndege kwa ajili ya kuwezesha Ndege kutua sa 24.
Maboresho mengoine ni pamoja na kituo cha kupokea nishati kwa maana ya maji na umeme, katika line ya umeme yenye msongo wa kilowatt 33 na lami ambayo inakidhi viwango na vigezo na yenye miundombinu toshelevu kwa ajili ya utuaji wa ndege.