Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

AIR TANZANIA YAANZA SAFARI ZA KWENDA AFRIKA KUSINI RASMI.

Imewekwa: 03 Dec, 2024
AIR TANZANIA YAANZA SAFARI ZA KWENDA AFRIKA KUSINI RASMI.

Shirika la ndege la Air Tanzania ATCL larejesha rasmi huduma ya usafiri wa moja kwa moja kutoka Tanzania hadi Afrika ya kusini lengo likiwa kuchochea Ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga na uchumi wa Taifa letu.

 

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa mara baada ya kuzindua safari hizo na kusema kuwa Serikali itaendelea kufanya uwekezaji kwenye Miundombinu ya Usafiri wa Anga ikiwemo  viwanja vya ndege na ununuzi wa mitambo ya kuongozea ndege na hali ya hewa.

 

"Serikali inaendelea kuboresha Miundombinu ya viwanja vya ndege nchini vikiwemo Iringa, Tanga, songea ,Mtwara, Musoma, na sumbawanga pia tunaenda kufungua nchi kibiashara ambapo kufikia sasa kuna mashirika makubwa ya ndege yanayotoa huduma kuunganisha Tanzania na nchi za kikanda na kimataifa. " Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

 

 

Waziri Prof. Mbarawa amesema katika jitihada za kuongeza mtandao wa safari kwa ATCL tayari Serikali  ya Jamhuri ya watu wa China imetoa kibali kwa Ndege ya mizigo ya Shirika hilo kupeleka mizigo Nchini humo.

 

Kwa upande wake Mhe. Balozi  John Ulanga kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki

Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa kurejeshwa kwa safari hizo kutarahisisha usafiri na biashara

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Air Tanzania Mhandisi  Peter Ulanga ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika ununuzi wa Ndege na kupitia ndege hizo  shirika litaweza kuunganisha nchi yetu na Nchi ya nje.