Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uchukuzi

WAZIRI MBARAWA ASISITIZA ULINZI MIPAKA YA VIWANJA

Imewekwa: 20 Nov, 2023
WAZIRI MBARAWA ASISITIZA ULINZI MIPAKA YA VIWANJA

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametoa siku mbili kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwaandikia notisi wananchi waliovamia eneo la Kiwanja cha Ndege cha Moshi ili kutokwamisha maboresho yanayoendelea kufanywa kiwanjani hapo

 

Akizungumza wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja hicho Mkoani Kilimanjaro Waziri Prof. Mbarawa amesema fidia zinazolipwa kwa wananchi wanoavamia maeneo ya miunondombinu zimekuwa zikiongeza gharama za ujenzi na hivyo kusababisha usumbufu kwa Makandarasi wakati wa utekeelezaji.

 

“Kuna miradi ambayo imechelewa kukamilika kwa sababu ya migogoro na wananchi ambao wakati mwingine wao ndio wamevamia maeneo ya Viwanja, kwa hapa hatuwezi kuwavumilia nakuagiza meneja kesho wananchi waliovamia wapewe barua ya kuvunja wenywe kabla Sheria hazichachukua mkondo wake’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.

 

Waziri Prof. Mbarawa amesema mipango ya Serikali Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu imeendelea kuboresha miundombinu ya Viwanja vya ndege nchini na kufufua upya shirika la ndege kwa kununua ndege ili kurahisisha shughuli za usafiri wa anga nchini.

 

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ameishukuru Serikali kuendelea kuboresha Viwanja vya ndege nchini kikiwemo na Kiwanja cha Moshi kwani kukamilika kwa kiwanja hicho kutachagiza shughuli za utalii mkoani humo.

 

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Motta Kyando amesema mradi wa Kiwanja cha Moshi unahusisha ujenzi wa maegesho ya ndege, njia za ndege, uzio wa usalama, mitaro na kalvati la kutolea maji, ujenzi wa eneo la Usalama, njia mbili ya kuruka kutua ndege na kwa sasa mradi umefikia asilimia 50.

 

Ujenzi wa Kiwanja cha Cha Kilimanjaro unatekelezwa na Mkandarasi M/s Rocktronic Limited kwa kiasi cha takribani bilioni 12 na unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2024