SEKTA YA UCHUKUZI YAENDELEA KUKUZA UCHUMI WA NCHI PROF KAHYARARA.
Sekta ya Uchukuzi inaendelea kukuza uchumi mkubwa nchini hivyo kupitia uchumi huo ni muhimu kwa wadau wote kuendelea kushirikiana na kutatua changamoto zilizopo.
Akizungumza Jijini Dar es salaam na wadau Mbalimbali Katibu Mkuu wizara ya uchukuzi Profesa Godius Kahyarara amesema kuwa kupitia kikao hiki kimewakutanisha wadau mbalimbali nchini wakiwemo TRA,TPA,Jeshi la Polisi, TAMISEMI, Wizara ya UchukuzI,DP World,TRC,TMA na TBS tunaenda kushirikiana kwa pamoja katika kuendeleza na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya uchukuzi.
"Aidha kupitia Sekta ya uchukuzi tuna ,Usafiri wa Njia ya Anga, Barabara, Maji na Reli ambapo inaleta mchango mkubwa katika uchumi wa nchi hivyo ni muhimu wadau kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo Mahususi." Alisema Prof Kahyarara".
Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Dar es salaam Abed Galus ameongeza kuwa kutokana na ongezeko wa Meli kubwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo shehena ya Mzigo umeongezeka na kuweza kuhudumia meli kubwa zinazobeba tani elfu sitini kwa wakati moja.
Hata hivyo Galus amesema kuwa Mamlaka ya bandari (TPA) kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kuboresha miundombinu ili kuondoa msongamano wa malori katika eneo la Bandari hiyo.
Naye Naibu katibu Mkuu kutoka TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila amesema hakuna haja ya kujenga mzani wa kupima magari katika Banadari Kavu ya Kwala hivyo magari yatumie Mzani wa Vigwaza na kupima katika bandari kavu ya kwala ili kuendelea kutumia mzani wa kuhamishika.
"Katika Hatua nyingine Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja amesema shirika la Reli Tanzania (TRC )linaendelea kuboresha vichwa vya Treni ili viweze kusafairisha mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kuelekea bandari kavu ya Kwala na Ihumwa Mkoani Dodoma.
Machibya amewataka wadau kuwekeza kwenye Treni kwani sheria kwani sheria inaruhusu sekta binafsi kumiliki treni ya mizigo na abiria.
